1Akatoka kule, akaenda kwao, alikokulia, nao wanafunzi wake wakamfuata.
2Ilipokuwa siku ya mapumziko, akaanza kufundisha katika nyumba ya kuombea, nao wengi waliomsikia wakashangaa, wakasema: Huyu haya ameyapata wapi? Werevu huu ulio wa kweli amepewa na nani? Hizo nguvu nazo zinazotendwa na mikono yake ni nguvu gani?Kufa kwa Yohana.(14-29: Mat. 14:1-2; Luk. 3:19-20; 9:7-9.)
14Mfalme Herode akayasikia, kwani Jina lake lilivuma, maana watu walisema: Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, kwa sababu hii nguvu hizo humtendesha kazi.
15Lakini wengine walisema: Ndiye Elia; wengine tena walisema: Ni mfumbuaji kama wale wafumbuaji wenzake.
16Lakini Herode alipoyasikia akasema: Ndiye Yohana, niliyemkata kichwa mimi, huyo amefufuka.
17Kwani Herode mwenyewe alikuwa ametuma kumkamata Yohana na kumfunga kifungoni kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa.
18Kwani Yohana alimwambia Herode: Ni mwiko kwako kuwa na mke wa nduguyo.Kulisha watu 5000.
35Saa zilipofika za jioni, wanafunzi wake wakamjia, wakasema: Hapa tulipo ni nyika, nazo saa zimefika za jioni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.