Matendo ya Mitume 28 - Swahili Roehl Bible 1937

Paulo aliyoyaona Melite.

1Tulipokwisha kuokoka, ndipo, tulipoambiwa, ya kuwa kisiwa kinaitwa Melite.

2Wenyeji wa huko wakatutunza kwa upendo usiopatikana kila siku: wakawasha moto, wakatupokea mwao sisi sote kwa ajili ya mvua iliyotunyea na kwa ajili ya baridi.Paulo na Wayuda wa Roma.

17Siku tatu zilipopita, akawakusanya wakubwa wa Wayuda. Walipokusanyika, akawaambia: Waume ndugu, mimi sikuwakosea wao wa ukoo wetu wala mazoea ya baba zetu. Nimefungwa huko Yerusalemu, nikatiwa mikononi mwa Waroma.

23Walipokwisha kuagana naye siku, wengi wakamjia huko, alikofikia, akawaeleza tangu asubuhi mpaka jioni akiushuhudia ufalme wa Mungu; tena akajaribu kuwashinda kwa ajili yake Yesu na kuwafumbulia maonyo ya Mose na maneno ya wafumbuaji wengine wakayaitikia maneno yake, wengine wakakataa kuyategemea.

24Wengine wakayaitikia maneno yake, wengine wakakataa kuyategemea.

25Hivyo wakashindwa kupatana wao kwa wao, wakajiendea zao. Ndipo, Paulo aliposema neno kwa kinywa cha mfumbuaji Yesaya:

26Nenda kwao wa ukoo huu, useme:

Kusikia mtasikia, lakini hamtajua maana;

Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.

27Kwani mioyo yao walio ukoo huu imeshupazwa,

wasisikie kwa masikio yao yaliyo mazito,

nayo macho yao wameyasinziza,

wasije wakaona kwa macho yao,

au wakasikia kwa masikio yao,

au wakajua maana kwa mioyo yao,

wakanigeukia, nikawaponya.

28Basi, ijulikane kwenu ninyi ya kwamba: Wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwenye wamizimu; hao ndio watakaousikia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help