Mashangilio 132 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuuombea Sioni.Wimbo wa kupapandia Patakatifu.

1Bwana, mkumbukie Dawidi masumbuko yake yote!

2Yeye alimwapia Bwana, kisha akamwagia naye yule Mwenye nguvu aliye Mungu wa Yakobo:

6Ndivyo, tulivyovisikia katika nchi ya Efurata, ndivyo, tulivyoviona mashambani kwenye misitu.1 Sam. 7:1; 2 Sam. 6:3.

7Na tuingie hapo, makao yake yalipo! Na tumwangukie hapo, anapowekea miguu yake!

8Inuka, Bwana, uingie penya kituo chako, wewe na Sanduku la Agano lenye nguvu zako,4 Mose 10:35; 2 Mambo 6:41-42.

9watambikaji wako wajivike wongofu, wakuchao washangilie!

10Kwa ajili ya mtumishi wako Dawidi usiurudishe nyuma uso wake yeye, uliyempaka mafuta.

11Bwana alimwapia Dawidi kiapo cha kweli, naye hatakiacha akirudi nyuma:Sh. 89:4.

12Walio uzao wa mwili wako nitawaketisha katika kiti chako cha kifalme, Kama wanao watalishika Agano langu, walifanye, kama watayashika hayo mashuhuda yangu, nitakayowafundisha, wana wao wataketi kale na kale katika kiti chako cha kifalme.

13Kwani Bwana aliuchagua mji wa Sioni, akaupenda, uwe Kao lake:Sh. 68:17; 76:3.

14Hapo ndipo, kitakapokuwa kituo changu cha kale na kale, hapo ndipo, nitakapokaa, kwani nimepapenda.

15Vilaji vyake nitavibariki, nao maskini wake nitawashibisha mikate.

16Watambikaji wake nitawavika wokovu, nao wanichao watapiga vigelegele.

17Hapo ndipo, nitakapolivumisha baragumu lake Dawidi, limpatie nguvu, naye, niliyempaka mafuta, nitamtengenezea taa.Sh. 89:25; 2 Sam. 7:16; Luk. 1:69.

18Walio adui zake nitawavika soni, lakini kichwani pake kitametameta kilemba, nilichomfunga.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help