1Fedha zina mahali pao zinapoonekana, nazo dhahabu zina mahali pao, wanapozifulia mitoni.
2Vyuma vinachimbuliwa uvumbini, tena yako mawe yanayotokea shaba kwa kuyeyushwa.
3Nalo giza mtu analikatia mpaka, ayachunguze mawe yaliyoko kule kuliko na giza lenyewe kwenye mlango wa kuzimu.
4Huko anachimbua shimo refu sana, kisha nayo njia ya ndani ya nchi pasipokaa watu; wanawahauliwa kwa kuwa chini ya hapo, watu wanapokanyaga; ndiko, wanakojiangika na kuning'inia, watu wengine wakiwa mbali.
5Nchi itoayo chakula juu chini yake inafudikizwa kwa kuchimbuliwa na nguvu zilizo sawa nazo za moto.
6Mahali pamojamoja huonekana mawe yenye almasi, pengine nayo madongo yenye dhahabu.
7Naye tai haijui njia hiyo, wala macho ya kozi hayajaiona kwa kuchungulia.
8Nyama wakali wenye majivuno hawajaikanyaga, wala simba mwenyewe hajaishika.
9Nayo mawe magumu yenyewe mtu huyavunja kwa mkono wake, hata milima anaifudikiza kwa kuichimbua toka misingini.
10Miambani anachonga njia za kupitia ndani yao; ndivyo, macho yake yanavyoona yote yaliyo yenye kima.
11Vijito vya ndani anaviziba, visimchuruzikie maji, apate kuyatokeza mwangani yaliyofichika ndani ya nchi.
12Lakini werevu wa kweli unaonekana wapi? napo mahali penye utambuzi pako wapi?
13Hakuna mtu ajuaye, unapotengenezwa, hauonekani katika nchi yao wenye uzima.
14Vilindi husema: Kwetu sisi hauko, nayo bahari husema: mimi nami sinao.
15Hata kwa dhahabu safi haupatikani, wala haulipiki kwa fedha kuwa bei yake,
20Je? Werevu wa kweli unatoka wapi? napo mahali penye utambuzi pako wapi?
21Umefichika machoni pao wote walio wenye uzima, nao ndege wa angani hawauoni, kwa kuwa uko umefunikwa.
22Kuzimu nacho kifo husema: Kwa masikio yetu tulisikia tu, ukitajwa.
23Mungu anaitambua njia ya kwenda kwake, yeye tu anapajua, hapo pake ulipo.Iyobu anasema na moyo wake kwa kuyakumbuka ya kale, aliyokuwa nayo.
Iyobu akaendelea kutoa mifano akisema:
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.