1Bwana akamwambia Mose: Nenda kwake Farao! Kwani mimi nimeushupaza moyo wake nayo mioyo ya watumishi wake, nipate kuvitoa hivi vielekezo vyangu katikati yao,
2kusudi wewe uyasimulie masikioni mwa mwanao namo mwa mjukuuu wako, niliyoyafanya huku Misri, navyo vilekezo vyangu, nilivyoviweka kwao, mpate kujua, ya kuwa mimi ni Bwana.
21Bwana akamwambia Mose: Uinue mkono wako na kuuelekeza mbinguni, katika nchi ya Misri kuwe giza jeusi sana la kupapaswa.
22Mose alipouinua mkono wake na kuuelekeza mbinguni, kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri siku tatu.
23Mtu hakuweza kumwona mwenziwe, wala mtu hakuondoka siku tatu mahali, alipokuwa. Lakini kwao wana wa Israeli kulikuwa na mwanga po pote, walipokaa.
24Ndipo, Farao alipomwita Mose, akamwambia: Nendeni kumtumikia Bwana! Mbuzi na kondoo na ng'ombe tu waachwe huku, lakini wana wenu na waende nayi!2 Mose 10:10.
25Mose akamwambia: Sharti wewe mwenyewe utupe mikononi mwetu ng'ombe za tambiko za kuchinja nazo za kuteketeza nzima, tupate za kumtolea Bwana Mungu wetu.
26Kwa hiyo, nayo makundi yetu sharti yaende nasi, lisisalie hata kwato moja. Kwani humo ndimo, tutakamochukua za kumtambikia Bwana Mungu wetu; kwani sisi hatujui, jinzi tutakavyomtumikia Bwana, mpaka tufike huko.
27Lakini Bwana akaushupaza moyo wa Farao, akatae kuwapa ruhusa kwenda zao.2 Mose 4:21.
28Kwa hiyo Farao akamwambia: Ondoka kwangu! Jiangalie, usitokee tena kuuona uso wangu! Kwani siku, utakapouona uso wangu, utakufa.
29Mose akajibu: Na viwe hivyo, ulivyosema, nisiuone tena uso wako mara nyingine.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.