1Katika wateule waliokuwamo Antiokia walikuwa wafumbuaji na wafunzi, akina Barnaba na Simeoni aliyeitwa Nigeri na Lukio wa Kirene na Manaeni aliyelelewa pamoja na mfalme Herode, tena Sauli.Elima.
4Kwa hivyo, walivyotumwa na Roho Mtakatifu, wakatelemka kwenda Seleukia; huko wakaingia chomboni kwenda Kipuro.
5Walipofika Salami wakalitangaza Neno la Mungu katika nyumba za kuombea za Wayuda. Naye Yohana alikuwa pamoja nao akiwatumikia.
34Lakini ya kuwa amemfufua katika wafu, asirudie tena kuoza, ndivyo, alivyosema kwamba:
Nitawapa ninyi magawio matakatifu ya Dawidi
yanayotegemeka.
41Ninyi wenye kubeza, angalieni na kustaajabu, mzizimke!
Kwani mimi siku hizi nitatenda tendo,
kama mtu angewasimulia tendo hilo, msingeliitikia.
42Walipotoka hapo, wamizimu wakawaomba, nao waambiwe maneno hayo siku ya pili ya mapumziko.
43Waliokuwamo nyumbani mwa kuombea walipotawanyika, Wayuda na wafuasi wengi waliomcha Mungu wakamfuata Paulo na Barnaba. Waliposema nao wakawahimiza, washikamane na magawio yake Mungu.Tume. 11:23.
44Siku ya mapumziko iliyofuata walikusanyika wao wa mji wote, walisikie Neno la Mungu.
45Lakini Wayuda walipoyaona hayo makundi ya watu wakajazwa wivu, wakayabisha yaliyosemwa na Paulo na kumtukana.Tume. 14:2; 13:50.
46Ndipo, Paulo na Barnaba waliposema waziwazi pasipo woga: Ilikuwa imepasa, ninyi mwambiwe wa kwanza Neno la Mungu. Lakini mnapolitupa na kujiwazia kwamba: Uzima wa kale na kale hauwafalii, basi, twawageukia wamizimu.Tume. 3:26; 28:25-28; Mat. 10:5-6; Luk. 7:30.
47Kwani tumeagizwa hivyo na Bwana:
Nimekuweka kuwa mwanga wa wamizimu,
uwe wokovu wao hata mapeoni kwa nchi.Yes. 49:6.
48Wamizimu walipoyasikia haya wakafurahi, wakalitukuza Neno la Bwana, wakalitegemea wote waliokuwa wamewekewa kupata uzima wa kale na kale.Rom. 8:29-30.
49Ndivyo, Neno la Bwana lilivyoenea katika nchi ile yote.
50Lakini Wayuda waliwachokoza wanawake wakuu walioyashika matambiko yao, hata wakubwa wa mji, wakawachukua, wawashambulie akina Paulo na Barnaba, wakawafukuza, watoke mipakani kwao.
51Ndipo, walipowakung'utia mavumbi ya miguuni, wakaenda, wakaja Ikonio.Tume. 18:6; Mat. 10:14; Luk. 9:5.
52Lakini wanafunzi wakajazwa furaha na Roho takatifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.