Mateo 24 - Swahili Roehl Bible 1937

Mambo yatakayokuja.(1-51: Mar. 13:1-37; Luk. 21:5-36.)

1Yesu alipotika Patakatifu akaenda zake. Wakamjia wanafunzi wake, wakamwonyesha majengo ya hapo Patakatifu;

2ndipo, alipojibu akiwaambia: Je? Mwayatazama haya yote? Kweli nawaambiani: Hapa halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.

3Kisha alipokaa mlimani pa michekele, wanafunzi wakamjia; walipokuwa peke yao wakasema: Tuambie, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo cha kurudi kwako na cha mwisho wa dunia ni nini?

4Yesu akajibu akiwaambia: Angalieni, mtu asiwapoteze!

5Kwani wengi watakuja kwa jina langu na kusema: Mimi ni Kristo; nao watapoteza wengi.

15*Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali Patakatifu, kama mfumbuaji Danieli alivyosema; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana!

29Maumivu ya siku zile yatakapopita, papo hapo jua litakuwa jeusi lenye giza, nao mwezi hautaumulikisha mwanga wake, nazo nyota zitaanguka toka mbinguni, nazo nguvu za mbingu zitatukutishwa.

32Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.

33Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo yote tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!

34Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo hayo yote.

35Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.

37Kama vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo kutakavyokuwa kurudi kwake Mwana wa mtu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help