Mifano 30 - Swahili Roehl Bible 1937

Ungamo la Aguri.Haya ni maneno ya Aguri, mwana wa Yake wa Masa.

1Mtu husema: Nimejisumbua, Mungu,

kweli nimejisumbua, Mungu, nikawezekana.

5Kila neno la Mungu ni nguvu,

ni ngao yao wamkimbiliao.Ombo la Aguri.

7Ninakuomba maneno haya mawili,

usininyime hayo, nikiwa ningaliko sijafa bado.

8Yaliyo upuzi na maneno ya uwongo yaweke mbali yasinifikie!

Usinipe kuwa mkosefu wa mali wala mwenye mali nyingi!

Ila nipe tu, nile chakula changu kinipasacho!

18Yako mambo matatu, ninayoyastaajabu sana,

tena yako manne, nisiyoyajua maana:Fano. 6:16.

19njia ya tai angani na njia ya nyoka mwambani

na njia ya merikebu baharini na njia ya mtu na mwanamwali.

20Ndivyo, njia ya mwanamke mgoni ilivyo:

hula, kisha hufuta kinywa chake na kusema: Sikukosa neno.

21Yako mambo matatu yanayoitetemesha nchi,

tena yako manne, nchi isiyoweza kuyavumilia:

22ni mtumwa akipata ufalme,

ni mpumbavu akishiba sana vyakula,Mbiu. 10:6.

23ni mwanamke aliyechukizwa akiolewa,

ni mjakazi akizipata mali za bibi yake, ziwe fungu lake.

24Wako nyama wanne walio wadogo katika nchi kuliko wengine,

nao ni werevu walioerevuka kweli.

25Ni siafu: kweli hawana nguvu,

lakini huvitengneza vyakula vyao siku za mavuno yao.Fano. 6:6-8; 10:5.

26Ni pelele: wao si wenye nguvu,

lakini huweka nyumba zao magengeni.

27Ni nzige: hawana mfalme,

lakini hutoka wote pia vikosi kwa vikosi.

28Ni mijusi: mtu anaweza kuwakamata kwa mikono,

lakini namo majumbani mwa wafalme wamo.

29Wako watatu wenye mwendo upendezao,

tena wako wanne wenye mwendo mzuri.

30Ni simba awapitaye nyama wote nguvu,

harudi nyumba kwa kuona cho chote.

31Ni farasi mwenye matandiko kiunoni, ni beberu naye,

tena ni mfalme akiviongoza vikosi vyake.

32Kama umepumbaa kwa kujikuza, au kama umewaza mabaya moyoni,

kifumbe kinywa kwa kukibandikia mkono!

33Kwa kusukasuka maziwa huleta siagi,

tena kuzidi kukamua pua hutoa damu,

nako kuchochea makali huleta ugomvi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help