1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, sema nao walio ukoo wako ukiwaambia: Kama ninailetea nchi panga, watu wa nchi hiyo watamchukua mtu mmoja miongoni mwao, wamweke kuwa mlinzi wao.
3Atakapoziona panga, zikiijia hiyo nchi, atapiga baragumu, awaonye wale watu.
4Lakini mtu akiisikiliza tu sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, panga zitamkamata, nayo damu yake atatwikwa yeye kichwani.
5Akiisikia sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, damu yake atatwikwa yeye, lakini yeye aonyekaye ataiponya roho yake.
6Lakini kama mlinzi anaona, panga zikija, asipige baragumu, watu hawaonyeki; basi, panga zikija, zikimkamata mtu mmoja tu wa kwao, yeye atakamatwa kwa ajili ya manza, alizozikora, lakini damu yake nitamlipisha mlinzi.
7Wewe nawe, mwana wa mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa mlango wa Isiraeli, utakaposikia neno kinywani mwangu, sharti uwaonye na kuwaambia hilo neno langu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.