2 Wafalme 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Ufalme wa Waisiraeli: Ugonjwa wa Ahazia.

1Ahabu alipokwisha kufa, Wamoabu wakawavunjia Waisiraeli maagano.Elia anaangusha moto toka mbinguni.

9Kisha mfalme akatuma kwake Elia mkuu wa kikosi cha hamsini pamoja na watu wake hamsini; alipopanda huko, aliko, akamwona, akikaa juu mlimani, akamwambia: Mtu wa Mungu, mfalme anakuagiza: Shuka!

10Lakini Elia akamjibu huyu mkuu wa hamsini na kumwambia: Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke toka mbinguni, ukule wewe na watu wako hamsini.Luk. 9:54; Ufu. 11:5.

11Akatuma tena kwake mkuu mwingine wa kikosi cha hamsini na watu wake hamsini, naye akasema na kumwambia: Mtu wa Mungu, ndivyo, mfalme anavyosema: Shuka upesi!

12Elia akawajibu kwamba: Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke toka mbinguni, ukule wewe na watu wako hamsini. Ndipo, moto uliposhuka toka mbinguni, ukamla na watu wake hamsini.

13Akatuma mara ya tatu mkuu wa kikosi cha hamsini na watu wake hamsini; huyu mkuu wa tatu wa kikosi cha hamsini alipopanda na kufika kwake akampigia Elia magoti, akamwambia na kumbembeleza: Mtu wa Mungu, roho yangu nazo roho za hawa watumishi wako hamsini usiziwazie kuwa si kitu!

14Tazama, moto ulishuka toka mbinguni, ukawala wale wakuu wa hamsini wawili wa kwanza na watu wao hamsini hamsini, sasa roho yangu usiiwazie kuwa si kutu!

15Ndipo, malaika wa Bwana alipomwambia Elia: Shuka naye, usimwogope! Basi, akaondoka, akashuka naye kwenda kwa mfalme.

Kufa kwake Ahazia.

16Akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa kuwa umetuma wajumbe kumwuliza Baali-Zebubu, mungu wa Ekroni, kama hakuna Mungu kwao Waisiraeli wa kumwuliza, atakavyosema, kwa sababu hii hutaondoka tena hapa kitandani, unapolala, ila utakufa kweli.2 Fal. 1:3-4.

17Akafa, kwa hilo neno la Bwana, Elia alilolisema; kisha Yoramuakawa mfalme mahali pake katika mwaka wa pili wa Yoramu, mwana wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, kwani Ahazia hakuwa na mwana.2 Fal. 3:1.

18Mambo mengine ya Ahazia, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help