1Kisha tukageuka, tukapanda na kushika njia ya Basani. Naye Ogi, mfalme wa Basani, akatoka, atujie yeye pamoja na watu wake wote, wapigane nasi kule Edirei.Mose anakatazwa kuingia Kanaani.
23Siku hizo nikambembeleza Bwana kwamba:
24Bwana Mungu wangu, wewe umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukuu wako na nguvu za mkono wako; kwani yuko Mungu gani mbinguni na duniani anayeweza kufanya matendo, kama hayo ya uwezo wako mwingi?
25Nipe ruhusa, nivuke, niione nchi hiyo njema iliyoko ng'ambo ya Yordani, hiyo milima mizuri, nayo ya Libanoni.
26Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, kwa hiyo Bwana hakunisika, akaniambia: Acha tu! Usiseme tena na mimi kwa ajili ya shauri hili!4 Mose 20:12.
27Panda juu mlimani kwa Pisiga, uyainue macho yako na kuyaelekeza upande wa baharini na wa kaskazini na wa kusini na wa maawioni kwa jua, uitazame hiyo nchi kwa macho yako. Kwani hutauvuka mto huu wa Yordani.
28Mwagizie Yosua mambo yako! Mtie nguvu na kumshikiza moyo! Kwani yeye ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, naye ndiye atakayewagawia nchi hiyo, utakayoiona, iwe yao.5 Mose 31:3,7.
29Kisha tukakaa bondeni na kuelekea Beti-Peori.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.