1Mungu akayasema maneno haya yote kwamba:
8Ikumbuke siku ya mapumziko kuitakasa!
9Siku sita sharti ufanye kazi, uyamalize mambo yako yote!
12Mheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!
18Nao watu wote walipoziona zile ngurumo na umeme na mlio wa baragumu nao mlima uliotoka moshi, walipoviona hivi vyote wakakimbia, wakasimama mbali,
19wakamwambia Mose: Sema wewe na sisi, nasi tutasikia! Lakini Mungu asiseme nasi, tusife.
20Naye Mose akawaambia: Msiogope! Kwani Mungu amekuja kuwajaribu ninyi, kusudi mwone na macho yenu, anavyoogopesha, mwache kumkosea.
21Kwa hiyo watu wakasimama mbali, lakini Mose akalikaribia lile wingu jeusi, Mungu alimokuwa.
Mungu anaagiza, jinsi watakavyomtambikia.22Bwana akamwambia Mose: Hivi ndivyo, uwaambie wana wa Isiraeli: Ninyi mmeona, ya kuwa nimesema nanyi toka mbinguni.Ebr. 12:18.
23Kwa hiyo msifanye vyo vyote kuwa Mungu kama mimi, msijifanyizie miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu!
24Unijengee kwa udongo pa kunitambikia, upate pa kunitolea ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukruni za kondoo wako na za ng'ombe wako! Napo po pote, nitakapokukumbusha Jina langu, nitakuja kwako, nikubariki.2 Mose 27:1-8; 29:42-43; 5 Mose 12:5.
25Nawe utakaponijengea kwa mawe pa kunitambikia, usitumie mawe ya kuchonga. Kwani ukiyapiga tu kwa chuma chako cho chote umekwisha kuyatia uchafu.5 Mose 27:5; Yos. 8:31.
26Tena usitumie ngazi ya kupapandia hapo pa kunitambikia, ni kwamba vyako vyenye soni visifunuliwe hapo pake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.