1Kisha Bwana akamwambia Yosua: Usiogope, wala usiingiwe na vituko! Wachukue watu wote kwenda vitani pamoja na wewe! Kisha ondoka kuupandia Ai! Tazama, nimemtia mfalme wa Ai mkononi mwako pamoja na watu wake na mji wake na nchi yake.
2Nawe uufanyizie Ai na mfalme wake, kama ulivyoufanyizia Yeriko na mfalme wake, vitu vyake tu mtakavyoviteka pamoja na nyama wao wa kufuga mtajichukulia, viwe mateka yenu. Jipatie penye kuuvizia mji upande wake wa nyuma!Yosua anawasomea watu wote Maonyo ya Mose.
30Kisha Yosua akajenga juu ya mlima wa Ebali pa kumtambikia Bwana.5 Mose 27:2-8.
31Kama Mose, mtumishi wa Bwana, alivyowaagiza wana wa Isiraeli, kama vilivyoandikwa katika kitabu cha Maonyo ya Mose, alipajenga pale pa kutambikia kwa mawe mazima yasiyochongwa kwa chuma cha mtu, akamtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wakachinja hata ng'ombe za tambiko za shukrani.
32Kisha akaandika hapo penye yale mawe mwandiko wa pili wa Maonyo ya Mose, aliouandika machoni pa wana wa Isiraeli.
33Nao Waisiraeli wote, wazee wao na wenye amri na waamuzi wao walikuwa wamesimama huku na huko penye lile Sanduku na kuwaelekea watambikaji Walawi waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana, wageni pamoja na wazalia, nusu yao waliuelekea mlima wa Gerizimu, nusu waliuelekea mlima wa Ebali, kama Mose, mtumishi wa Bwana, alivyowaagiza kale kuubariki ukoo wa Waisiraeli.5 Mose 11:29; 27:12-13.
34Baadaye akayasoma maneno yote ya Maonyo, ya mbaraka nayo ya kiapizo, sawasawa kama yalivyoandikwa katika kitabu cha Maonyo.
35Katika yale yote, Mose aliyoyaagiza, halikuwamo hata moja, Yosua asilolisoma masikioni pa mkutano wa Waisiraeli wote, wakiwa pamoja na wanawake na wana wa wageni waliokwenda kukaa nao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.