Mashangilio 47 - Swahili Roehl Bible 1937

Mungu wa Isiraeli ni mfalme wa makabila yote.Kwa mwimbishaji. Wimbo wa wana wa Kora.

1Makabila yote ya watu, pigeni makofi! Mwimbieni Mungu kwa shangwe na kumpigia vigelegele!

2Kwani Bwana alioko huko juu huogopesha, ni mfalme mkubwa azitawalaye nchi zote.

3Aliteka makabila ya watu, watutii, nazo koo nzima, zituangukie miguuni.

4Akatuchagulia fungu, liwe letu; ndilo, mpendwa wake Yakobo ajivunialo.

5Mungu alipaa na kushangiliwa, Bwana ndiye aliyepigiwa baragumu.

8Mungu anawatawala wamizimu nao, Mungu anakaa katika kiti chenye utakatifu wake.

9Wakuu wa makabila ya watu wamekusanyika, wawe ukoo wa Mungu wa Aburahamu, kwani ngao za hapa chini ni zake Mungu, ametukuka sanasana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help