1Mose pamoja na wazee wa Waisiraeli wakawaagiza watu kwamba: Yaangalieni maagizo yote, mimi ninayowaagiza leo!
16Na awe ameapizwa atakayembeza baba yake na mama yake! Nao watu wote na waitikie: Amin!
17Na awe ameapizwa atakayeusogeza mpaka wa mwenzake! Nao watu wote na waitikie: Amin!
18Na awe ameapizwa atakayempoteza kipofu njiani! Nao watu wote na waitikie: Amin!
19Na awe ameapizwa atakayepotoa shauri la mgeni au la mwana aliyefiwa na wazazi au la mjane! Nao watu wote na waitikie: Amin!
20Na awe ameapizwa atakayelala na mkewe baba yake! Kwani huko atazifunua nguo za baba yake. Nao watu wote na waitikie: Amin!
24Na awe ameapizwa atakayempiga mwenzake mahali panapojificha! Nao watu wote na waititike: Amin!
25Na awe ameapizwa atakayechukua mapenyezo, ampige mtu na kuimwaga damu yake asiyekosa! Nao watu wote na waitikie: Amin!
26Na awe ameapizwa asiyeyasimamisha maneno ya Maonyo haya na kuyafanya! Nao watu wote na waitikie: Amin!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.