Mashangilio 119 - Swahili Roehl Bible 1937

Utukufu wa Neno lake Bwana.

1Wenye shangwe ndio wao wanaofuata njia zisizokosesha, wanaoendelea kuyafuata Maonyo yake Bwana.

17Mtendee mema mtumishi wako, nipate uzima tena! Na nilishike Neno lako na kulifuata!

18Yafumbue macho yangu, nipate kuona, niyaone mataajabu yatokeayo kwenye Maonyo yako.

19Mimi ni mgeni katika nchi, usinifiche maagizo yako!

25Ambayo roho yangu imegandamana nayo, ndiyo mavumbi; kwa hivi nirudishe uzimani, kama ulivyosema!

26Nilipokusimulia, njia zangu zilivyo, uliniitikia; unifundishe maongozi yako, niyajue!

27Unitambulishe njia ya amri zako, niyawaze mataajabu yako!

28Roho yangu imeyeyuka kwa ukiwa; niinue, kama ulivyosema!

29Njia ya uwongo ipitishe mbali, nisiione! Kwa huruma zako nipe kuyashika Maonyo yako!

30Njia yenye kweli ndiyo, niliyoichagua, maamuzi yako nimeyaweka machoni pangu.

31Ambayo nimegandamana nayo, ndiyo mashuhuda yako; Bwana, usiniache, nikatwezwa!

32Nitapiga mbio, nifike njiani kwa maagizo yako, kwani moyo wangu umeupatia mahali papana.

33Nifunze, Bwana, niijue njia ya maongozi yako, niishike na kuifuata mpaka mwisho!

34Nitambulishe Maonyo yako, niyashike, niyaangalie na kuyafuata kwa moyo wote.

35Niendeshe katika mkondo wa maagizo yako! Kwani yanayonipendeza ndiyo hayo.

65Mtumishi wako umemfanyizia mema, kama ulivyosema, Bwana.

73Mikono yako iliniumba na kunitengeneza; nipe kuvitambua, nijifundishe maagizo yako!

74Wakuogopao hufurahi wakiniona mimi, kwani Neno lako ndilo, ninalolingojea.

75Nimeyajua maamuzi yako, Bwana, kuwa yenye wongofu, maana umeninyenyekeza kwa welekevu.

89Bwana, Neno lako ni la kale na kale, lilitiwa nguvu kule mbinguni.

161Wao walionikimbiza bure ndio wakuu, lakini moyo wangu unaloliogopa sana, ni Neno lako.

162Mimi ninayafurahia, uliyoyasema, kama mtu atokaye vitani mwenye mateka mengi.

163Uwongo nimeuchukia, hunitapisha; Maonyo yako ndiyo, ninayoyapenda.

164Ninakushangilia kila siku mara saba zote kwa ajili ya wongofu wako wa kuamulia watu.

165Wayapendao Maonyo yako hupata utengemano mwingi, hawaoni lo lote litakalowakwaza.

166Bwana, wokovu wako nimeutazamia, nayo maagizo yako nimeyafanya.

169Malalamiko yangu na yakufikie karibu usoni pako, Bwana! Kama ulivyosema, nipe utambuzi!

170Maombo yangu na yakujie usoni pako! Kama ulivyoniambia, uniponye!

171Shangwe na zifurike midomoni mwangu, kwa kuwa ulinifundisha maongozi yako!

172Ulimi wangu na uliitikie Neno lako! Kwani maagizo yako yote ni yenye wongofu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help