1Hapo, walipoukaribia Yerusalemu na kufika Beti-Fage na Betania penye mlima wa michekele, akatuma wanafunzi wake wawili,
2akawaambia: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mara mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete!
3Kama mtu atawauliza: Mbona mnafanya hivi? semeni: Bwana wetu anamtakia kazi! Mara atawapani, mmlete hapa.Kuwafukuza wachuuzi Patakatifu.
15Walipofika Yerusalemu, akapaingia Patakatifu, akaanza kuwafukuza wenye kuuzia na kununulia hapo Patakatifu, akaziangusha meza za wavunja fedha na viti vya wachuuzi wa njiwa.
16Tena hakuacha, mwenye kuchukua chombo apapitie hapo Patakatifu.
17Akawafundisha akiwaambia: Haikuandikwa ya kuwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya kuombea kwao makabila yote ya watu? Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.Ubatizo wa Yohana.(27-33: Mat. 21:23-27; Luk. 20:1-8.)
27Walipoingia tena Yerusalemu, naye alipotembea Patakatifu, wakamjia watambikaji wakuu na waandishi na wazee,
28wakamwuliza: Hayo unayafanya kwa nguvu gani? au ni nani aliyekupa nguvu hii, uyafanye hayo?
29Yesu akawaambia: Nanyi nitawauliza neno moja; mtakaponijibu, nitawaelezea nguvu yangu ya kuyafanya hayo.
30Ubatizo wake Yohana ulitoka mbinguni au kwa watu? Nijibuni!
31Wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea?
32Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, basi, waliwaogopa watu; kwani watu wote walimshika Yohana kuwa mfumbuaji wa kweli.
33Kwa hiyo wakamjibu Yesu wakisema: hatujui. Ndipo, Yesu alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.