Matendo ya Mitume 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Petero na Yohana mbele ya wakuu.

1*Walipokuwa wakisema na watu, wakawajia watambikaji na mlinda Patakatifu na Masadukeo.

5Kulipokucha, wakakusanyika Yerusalemu wakubwa wao na wazee na waandishi

6na mtambikaji mkuu Ana na Kayafa na Yohana na Alekisandro nao wote waliokuwa wa ukoo wa mtambikaji mkuu.

7Kisha wakawasimamisha katikati, wakawauliza: Hilo ninyi mmelifanya kwa nguvu ya nani au kwa jina la nani?

26Mbona makabila ya watu huwaza mambo yaliyo ya bure?

Wafalme wa nchi hushikana mioyo?

wakuu nao hula njama wakikaa pamoja,

wamkatae Bwana na Kristo wake.

27Hii ni kweli, kwani walikusanyika mjini humu, wamkamate mtoto wako mtakatifu Yesu, uliyempaka mafuta; akina Herode na Pontio Pilato walipatana na wamizimu na watu wa Isiraeli,Luk. 23:12.

28wayafanye yote, uliyomtakia kale kwa mkono wako na kwa mapenzi yako, kwamba yatimie papo hapo.Tume. 2:23.

29Na sasa, Bwana, yatazame matisho yao! Wape watumwa wako waliseme Neno lako waziwazi pasipo woga hata kidogo!Ef. 6:19.

30Unyoshe mkono, uponye watu na kufanya vielekezo na vioja kwa Jina la mtoto wako mtakatifu Yesu!

31Walipoomba hivyo, hapo, walipokuwa wamekusanyika, pakatetemeka, wakajazwa wote Roho Mtakatifu, wakalisema Neno la Mungu waziwazi pasipo woga.

32*Nao wigi wa watu waliokuwa wamemtegemea Bwana, mioyo yao nazo roho zao zilikuwa moja; tena hakuwako hata mmoja aliyezitumia mali zake, kama ni zake mwenyewe, lakini vyote walivitumia bia.Tume. 2:44.

33Nao mitume wakaushuhudia ufufuko wa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi, magawio makuu ya Mungu yakiwakalia wao wote.Tume. 2:47.

34Kwa hiyo hakupatikana kwao aliyekosa vitu, alivyopaswa navyo. Kwani wote waliokuwa wenye mashamba au nyumba waliziuza,Tume. 2:45.

35wakaziweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa, kama alivyokosa.*

36Kulikuwa na Mlawi aliyetoka Kipuro, jina lake Yosefu, aliyeitwa na mitume Barnaba, maana yake Mwana wa Tulizo,Tume. 11:22,24.

37naye alikuwa na shamba, akaliuza, akazileta fedha, akaziweka miguuni pa mitume.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help