1Siku ya Pentekote (Hamsini) ilipotimia, wote walikuwa pamoja mahali palepale pamoja.
5Mle Yerusalemu walikuwamo wakikaa Wayuda wenye kumcha Mungu wa kila taifa lililoko chini ya mbingu.
22Enyi waume wa Kiisiraeli, yasikilizeni maneno haya! Yesu wa Nasareti alikuwa amejulikana, kwamba ametoka kwa Mungu hapo alipokuja kwenu na kufanya vya nguvu na vioja na vielekezo, tena ni Mungu aliyempa kuvifanya machoni penu, kama mnavyojua wenyewe.
23Kwa kuwa Mungu alikuwa amempatia kazi na kumkatia mpaka kwa vile, anavyovijua vyote, vikiwa havijatimia bado, kwa hiyo ametolewa, mkampata mikononi mwa wapotovu, mkamwua na kumwamba msalabani.
26Kwa hiyo moyo wangu hufurahi,
nao ulimi wangu hushangilia;
hata mwili wangu utatulia kwa kuwa na kingojeo.
27Kwani hutaiacha roho yangu, ipotee kuzimuni,
wala hutamtoa akuchaye, apate kuoza kaburini.
28Unanitambulisha njia ziendazo penye uzima,
utanijaza furaha zilizopo usoni pako.
29Waume ndugu zangu, mnipe ruhusa, niseme kwenu waziwazi: Dawidi aliye babu yetu mkuu alikufa, akazikwa, nalo kaburi lake liko kwetu hata siku hii ya leo.
35Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu,
mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
36Kwa hiyo wote walio wa mlango wa Israeli watambue kweli: Huyo Yesu, mliyemwamba msalabani ninyi, Mungu amemfanya, awe Bwana na Kristo!
37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyoni, wakamwambia Petero na mitume wengine: Waume ndugu zetu, tufanyeje?
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.