2 Wafalme 23 - Swahili Roehl Bible 1937

Yosia anafanya agano jipya na Mungu.(Taz. 2 Mambo 34:29—36:5.)

1Ndipo, mfalme alipotuma wajumbe, wakusanye kwake wazee wote wa Wayuda na wa Yerusalemu.

2Kisha mfalme akapanda kwenda Nyumbani mwa Bwana pamoja na Wayuda wote na wenyeji wote wa Yerusalemu na watambikaji na wafumbuaji na watu wote pia, wadogo kwa wakubwa, wakaenda naye, akawasomea masikioni pao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichooneka Nyumbani mwa Bwana.

3Kisha mfalme akaja kusimama penye ile nguzo, akafanya mbele ya Bwana agano la kumfuata Bwana na kuyaangalia maagizo yake na mashuhuda yake na maongozi yake kwa moyo wote na kwa roho yote, ayasimamishe maneno ya Agano hili yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Nao watu wote wakaliitikia agano hili, walishike na kulisimamia.Yosia anayaondoa matambiko ya kimizimu.

4Kisha mfalme akamwagiza mtambikaji mkuu Hilkia na watambikaji wa pili na walinzi wa vizingiti, watoe Jumbani mwa Bwana vyombo vyote vilivyotengenezwa vya kumtambikia Baali na Ashera na vikosi vyote vya mbinguni, wakavichoma moto nje ya Yerusalemu kwenye mashamba ya Kidoroni, nayo majivu yao akayatuma kupelekwa Beteli.Kufa kwake Yosia.

28Mambo mengine ya Yosia nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?

29Hizo siku zake akapanda Farao Neko, mfalme wa Misri, kwenda kupigana na mfalme wa Asuri kwenye mto wa Furati. Mfalme Yosia alipotoka kumpinga, yule akamwua kule Megido papo hapo, alipomwona.

30Watumishi wake wakamchukua garini, alipokwisha kufa, wakamtoa Megido na kumpeleka Yerusalemu, wakamzika kaburini mwake. Kisha watu wa nchi hii wakamchukua Yoahazi, mwana wa Yosia, wakampaka mafuta, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake.Mfalme Yoahazi.

31Yoahazi alikuwa mwenye miaka 23 alipoupata ufalme, akawa mfalme miezi 3 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Hamutali, binti Yeremia, wa Libuna.

32Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, baba zake waliyoyafanya.

33Farao Neko akamfunga huko Ribula katika nchi ya Hamati, asiwe mfalme mle Yerusalemu, akailipisha nchi hii vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000, na kipande kimoja cha dhahabu, ndio shilingi 220000.Mfalme Yoyakimu.

34Kisha Farao Neko akamfanya Eliakimu, mwana wa Yosia, kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, akaligeuza jina lake, akamwita Yoyakimu. Lakini Yoahazi akamchukua, aje naye Misri; ndiko, alikokufa.

35Zile fedha na dhahabu Yoyakimu akampa Farao; lakini hakuwa na budi kuitoza nchi machango, apate kuzilipa hizo fedha, Farao alizozitaka; watu wa hiyo nchi yake akamtoza kila mmoja kwa mali, alizowaziwa kuwa nazo; ndivyo, alivyowachangisha hizo fedha na dhahabu za kumpa Farao Neko.2 Fal. 15:20.

36Yoyakimu alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Zebuda, binti Pedaya, wa Ruma.

37Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, baba zake waliyoyafanya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help