1Siku ile Yesu alitoka nyumbani, akaenda kukaa kandokando ya bahari.
2Wakamkutanyikia makundi mengi ya watu, kwa hiyo akaingia chomboni, akakaa humo, watu wote wakisimama pwani.
3Akawaambia maneno mengi kwa mifano akisema: Tazameni, mpanzi alitoka kumiaga mbegu.
4Ikawa alipozimiaga, nyingine zikaangukia njiani; ndege wakaja, wakazila.
5Nyingine zikaangukia penye miamba pasipo na udongo mwingi. Kuota zikaota upesi kwa kuwa na udongo kidogo;
6lakini jua lilipokuwa kali, zikanyauka, kwa kuwa hazina mizizi.
7Nyingine zikaangukia penye miiba; nayo miiba ilipoota ikazisonga.
8Lakini nyingine zikaangukia penye mchanga mzuri, zikazaa, nyingine punje mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.
9Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
Sababu ya kusema kwa mifano.10Wanafunzi wake wakamjia, wakamwambia: Sababu gani unasema nao kwa mifano?
11Naye akajibu akisema: Ninyi mmepewa kuyatambua mafumbo ya ufalme wa mbingu,Kipunje cha haradali.(31-32: Mar. 4:30-32; Luk. 13:18-19.)
31*Akawatolea mfano mwingine akisema: Ufalme wa mbingu umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukipanda katika shamba lake.
32Nacho ni kidogo kuliko mbegu zote. Lakini kinapokua ni mkubwa kuliko miboga yote inayopandwa, huwa mti mzima, hata ndege wa angani huja na kutua katika matawi yake.
Chachu.33Akawaambia mfano mwingine: Ufalme wa mbingu umefanana na chachu, mwanamke akiitwaa akaichanganya na pishi tatu za unga, mpaka ukachachwa wote.
36Kisha Yesu akawaaga makundi ya watu, akaingia nyumbani. Ndipo, wanafunzi wake walipomjia wakisema: Tuelezee mfano wa nyasi za shambani!Fedha katika shamba.
44*Ufalme wa mbingu umefanana na fedha zilizofukiwa shambani. Mtu alipoziona akazifukia, akaenda kwa furaha yake, akaviuza vyote, alivyokuwa navyo, akalinunua shamba lile.
45Tena ufalme wa mbingu umefanana na mchuuzi aliyetafuta ushanga wa lulu nzuri.
46Naye alipoona lulu moja yenye bei kubwa akaenda, akaviuza vyote alivyokuwa navyo, akainunua.*Wavu wa kuvulia samaki.
47Tena ufalme wa mbingu umefanana na wavu uliotupwa baharini, ukakusanya samaki wa kila mtindo.Mat. 22:9-10.
48Hata ulipojaa, wakauvuta pwani, wakakaa, wakawachagua samaki, walio wazuri wakawaweka vyomboni, lakini walio wabaya wakawatupa.
49Hivyo ndivyo, itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii: Malaika watatokea, watawatenga wabaya kati ya waongofu,Mat. 25:32.
50wawatupe shimoni mwa moto. Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
51Mmeijua maana ya hayo yote? Walipomwambia: Ndio,
52akawaambia: Kwa sababu hii kila mwandishi aliyefundishiwa ufalme wa mbingu amefanana na mtu mwenye nyumba anayetoa mawekoni mwake mambo mapya na ya kale.
Yesu mjini mwa Nasareti.(53-58: Mar. 6:1-6; Luk. 4:15-30.)53Ikawa, Yesu alipokwisha kuisema mifano hiyo akatoka, akaenda zake.
54Alipofika kwao, alikokulia, akawafundisha katika nyumba yao ya kuombea, nao wakashangaa wakisema: Huyu amepata wapi werevu huu ulio wa kweli na nguvu hizi?
55Huyu si mwana wa seremala? Mama yake si yeye anayeitwa Maria? Nao ndugu zake sio akina Yakobo na Yosefu na Simoni na Yuda?
56Nao maumbu zake hawako wote kwetu? Basi, huyu amepata wapi haya yote? Wakajikwaa kwake.Yoh. 7:15,52.
57Yesu akawaambia: Mfumbuaji habezwi, isipokuwa kwao, alikokulia, namo nyumbani mwake.Yoh. 4:44.
58Kwa hiyo hakufanya kule ya nguvu mengi, kwa sababu walikataa kumtegemea.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.