1Maombo ya mnyonge; kwa kufikisha kuzimia roho anamtolea Bwana wasiwasi wake.
2Bwana, lisikilize ombo langu! Kilio changu sharti kifike kwako wewe.
3Usiufiche uso wako, nisiuone ninaposongeka! Nitegee sikio lako, ninapokuita, uniitikie upesi!
4Kwani siku zangu hupotea kama moshi, nayo mifupa yangu huchomwa kama vijinga vya moto.
5Moyo wangu umeungua, ukanyauka kama majani, kwa hiyo mimi husahau kula chakula changu.
6Kwa hivyo, ninavyolia na kupiga kite, nyama za mwili wangu zimegandamana nayo mifupa.
24Njiani alizipunguza nguvu zangu, nazo siku zangu akazifupiza.
25Nikasema: Mungu wangu, usiniondoe, siku zangu simefika kati tu! Miaka ikaayo kwa vizazi na vizazi ni yako wewe.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.