1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, utegee mlango wa Isiraeli kitendawili na kuuambia fumbo!
3Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kulikuwako tai mkubwa mwenye mabawa makubwa na manyoya marefu mabawani ya kumwendesha, nayo mengi mno yalikuwa yenye rangi; huyo akaja Libanoni, akajichukulia kilele cha mwangati.
4Chipuko lake la juu penyewe akalivunja, akalipeleka katika nchi yenye biashara, akalitia mjini, wachuuzi wakaamo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.