1Palikuwa pamesalia siku mbili kuwa sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Nao watambikaji wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata kwa werevu, wapate kumwua;
2lakini walisema: Kwanza sikukuu ipite, watu wasije, wakafanya fujo!
Yesu anamiminiwa mafuta.(3-9: Mat. 26:6-13; Yoh. 12:1-8.)3Naye alipokuwa Betania nyumbani mwa Simoni Mkoma akikaa chakulani, akamjia mwanamke mwenye kichupa chepe cha jiwe kilichojaa mafuta ya maua yanayoitwa Narada; ni yenye bei kubwa, nayo yalikuwa hayakuchanganywa na mengine. Akakivunja kile kichupa, akayamiminia kichwani pake.Getisemane.(32-42: Mat. 26:36-46; Luk. 22:40-46.)
32Walipofika mahali, jina lake Getisemane, akawaambia wanafunzi wake: Kaeni hapa, mpaka niishe kuomba!Kukamatwa kwa Yesu.(43-54: Mat. 26:47-58; Luk. 22:47-55; Yoh. 18:2-18.)
43Angali akisema, papo hapo akaja Yuda, mmoja wao wale kumi na wawili, pamoja na kundi la watu wengi wenye panga na rungu waliotoka kwa watambikaji wakuu na kwa waandishi na kwa wazee.
44Lakini mwenye kumchongea alikuwa amewapa kielekezo akisema: Nitakayemnonea ndiye, mkamateni, mwende naye mkimwangalia sana!
45Naye alipofika, mara akamjia, akasema: Mfunzi mkuu! akamnonea;
46ndipo, walipomkamata kwa mikono yao.
47Lakini mmoja wao waliosimama hapo akauchomoa upanga wake, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio.
48Lakini Yesu akajibu, akawaambia: Mmetoka wenye panga na rungu, mnikamate mimi, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi.
49Kila siku nilikuwa kwenu hapo Patakatifu nikifundisha, lakini hamkunikamata; lakini yamekuwapo, Maandiko yatimizwe.
50Hapo waliokuwa naye wakamwacha, wakakimbia wote.
51Kulikuwa na kijana mmoja aliyefuatana naye, alikuwa ameufunika uchi wake kwa kitambaa cha bafta tu. Lakini walipomkamata,
52akakiacha kile kitambaa cha bafta, akakimbia mwenye uchi.
Yesu mbele ya Kayafa.53Wakampeleka Yesu kwa mtambikaji mkuu. Wakakusanyika wote, watambikaji wakuu na wazee na waandishi.
54Naye Petero akamfuata mbalimbali, mpaka akaingia uani kwa mtambikaji mkuu, akakaa pamoja na watumishi penye mwangaza akiota moto.
(55-65: Mat. 26:59-68; Luk. 22:63-71; Yoh. 18:19-24.)55Lakini watambikaji wakuu na baraza ya wakuu wote wakamtafutia Yesu ushuhuda, wapate kumwua, lakini hawakuupata.
56Kwani wengi walimshuhudia ya uwongo, lakini ushuhuda wao haukupatana.
57Kisha wakainuka wengine, wakamshuhudia ya uwongo na kusema:
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.