Yohana 17 - Swahili Roehl Bible 1937

Maombo ya Yesu.

1Yesu alipokwisha kuyasema haya akayaelekeza macho yake mbinguni, akasema: Baba, saa imekwisha fika. Mtukuze Mwana wako, Mwana wako naye akutukuze!

2Ni kama hivyo, ulivyompa kumtawala kila mwenye mwili, awape wote, uliompa, uzima wa kale na kale.Kuwaombea wanafunzi.

6Jina lako nimewafumbulia watu, ulionipa na kuwatoa ulimwenguni. Walikuwa wako, nawe umenipa mimi, nalo Neno lako wamelishika.Kuwaombea Wakristo wote.

20Lakini si hawa tu, ninaowaombea, ila nawaombea hata wale watakaonitegemea wakilisikia neno lao.

21Wote wapate kuwa mmoja, kama ulivyomo mwangu, wewe Baba, nami nilivyomo mwako! Wapate kuwamo mwetu nao hao, ulimwengu upate kunitegemea, ya kuwa wewe umenituma.Gal. 3:28.

22Nami nimewapa utukufu, ulionipa wewe, wapate kuwa mmoja, kama sisi tulivyo mmoja.Tume. 4:32.

23Mimi niwemo mwao, nawe wewe uwemo mwangu, wawe watu waliomaliza kuwa mmoja, nao ulimwengu utambue, ya kuwa wewe umenituma, kisha umewapenda, kama ulivyonipenda mimi.1 Kor. 6:17.

24Baba, nataka hata wale, ulionipa, wawe pamoja nami papo hapo, nitakapokuwapo mimi, wapate kuuona utukufu wangu, ulionipa, kwa sababu umenipenda, ulimwengu ulipokuwa haujaumbwa bado.Yoh. 12:26.

25Baba mwongofu, ulimwengu haukukutambua, lakini mimi nimekutambua, nao hao wametambua, ya kuwa wewe umenituma.

26Nami nimewatambulisha Jina lako, na tena nitalitambulisha, kwamba upendo, wewe ulionipenda, uwakalie, nami niwemo mwao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help