Matendo ya Mitume 8 - Swahili Roehl Bible 1937

Mafukuzo ya Wakristo.

1Sauli naye alikuwa amependezwa na kuuawa kwake. Siku ile wateule waliokuwamo Yerusalemu wakashambuliwa na kufukuzwa kabisa; kwa hiyo wote wakatawanyika katika nchi za Yudea na za Samaria; waliosalia ni mitume tu.Filipo.

4Wale waliotawanyika wakapita huko na huko wakiipiga mbiu njema ya lile Neno.

5Filipo akashuka kuuingia mji wa Samaria, akawapigia mbiu ya Kristo;Mganga Simoni.

9Kulikuwa na mtu mjini mle, jina lake Simoni, aliyekuwa akiwahangaisha watu wote wa Samaria kwa uganga wake akijisemea mwenyewe: Mimi ni mwenye uwezo.

10Wote, wadogo hata wakubwa, wakashikamana naye wakisema: Huyu ndio uwezo wa Mungu unaoitwa mkuu.

11Lakini walishikamana naye, kwa sababu aliwahangaisha siku nyingi kwa uganga wake.

12Lakini walipomtegemea Filipo aliyewapigia mbiu njema ya ufalme wa Mungu na ya Jina la Yesu Kristo, wakabatizwa, waume na wake.

33Kwa hivyo, alivyonyenyekea, alinyimwa uamuzi mnyofu;

yuko nani atakayesimulia, ukoo wake ulivyokuwa?

Kwani ameondolewa katika nchi yao walio hai, asikae nchini.

34Mtunza mali akamwuliza Filipo akisema: Nakuomba, uniambie: Haya mfumbuaji anayasema ya nani? Anajisema mwenyewe au anamsema mwingine?

35Ndipo, Filipo alipokifumbua kinywa chake, akaanza kwa Maandiko yale yale akimpigia mbiu ya Yesu.

36Walipoendelea njiani wakafika penye maji kidogo, mtunza mali akasema: Tazama, yako maji, iko nini tena inayozuia, nisibatizwe?

37Filipo akasema: Ukimtegemea Bwana kwa moyo wako wote, inawezekana. Ndipo, alipojibu akisema: Namtegemea Yesu Kristo kuwa Mwana wake Mungu;

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help