Mashangilio 55 - Swahili Roehl Bible 1937

Kilio cha mtu asongekaye sana.

1Kwa mwimbishaji. Fundisho la Dawidi la kuimbia mazeze.

2Sikiliza Mungu, kuomba kwangu!

Usijifiche, nikikulalamikia!

3Niangalie, uniitikie! Ninahangaika kwa kulia kwangu na kupiga kite.

4Kwa sababu adui wananizomea, nao wasiomcha Mungu wananisonga, kwani wanataka, mateso yaniangukie, kwa ukali tu wananipingia.

5Moyo wangu humu ndani yangu unatetemeka, mastuko kama ya kufa yakaniguia;

6masukosuko ya mwili yananijia kwa kuogopa tu, nikapigwa sana na bumbuazi.

7Nikasema: Ningepata mabawa kama ya njiwa, ningeruka na kutua pawapo pote!

17Mimi ninamlilia Mungu, yeye Bwana ataniokoa.

18Jioni na mapema na mchana kutwa na nilalamike na kupiga kite; ndipo, atakapoisikia sauti yangu.

19Ataikomboa roho yangu, nikae na kutengemana, wao wasinifikie, ijapo wawe wengi wanaonijia;

20Mungu husikia, naye atawajibu. Yeye ndiye akaaye tangu kale. Wao hawataki kugeuka, kwa kuwa hawamwogopi aliye Mungu.

21Maana wanawakamata nao waliomkalia Mungu, nalo Agano lake wanalipinga.

22Wayasemayo ni mafuta ya midomo, ni matamu kuliko maziwa, lakini mioyoni mwao huwaza vita. Maneno yao, wayasemayo, hulegea kuliko mafuta ya uto, lakini wenyewe ndio panga zilizokwisha kuchomolewa.

23Umtupie bwana yakulemeayo! Yeye atakumalizia, hatamtoa mwongofu, atikisike kale na kale.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help