Marko 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Mgerasi mwenye pepo.(1-21: Mat. 8:28-34; Luk. 8:26-40.)

1Wakafika ng'ambo ya bahari katika nchi ya Wagerasi.

2Alipotoka chomboni papo hapo akakutana na mtu mwenye pepo mchafu aliyetoka penye makaburi.

3Kwa kuwa hukaa pale penye makaburi, hakuwako mtu aliyeweza kumfunga kwa mnyororo wo wote.

4Kwani alikuwa amefungwa mara nyingi kwa mapingu na kwa minyororo, lakini minyororo ikararuliwa naye, nayo mapingu yakasagwa naye, mpaka yakikatika, kwa hiyo hakukuwako kabisa mtu mwenye nguvu za kumshinda.

5Siku zote mchana kutwa alikuwa penye makaburi nako milimani akipiga makelele na kujipigapiga mawe mwenyewe.

6Alipomwona Yesu, yuko mbali bado, akapiga mbio, akaja, akamwangukia,

7akapaza sana sauti akisema: Tuko na jambo gani mimi na wewe Yesu, Mwana wa Mungu Alioko huko juu? Nakuapisha kwa Mungu, usiniumize!Binti Yairo.

21Yesu alipokwisha vuka tena chomboni kuja ng'ambo, kundi la watu wengi likakusanyika hapo, alipokuwa kandokando ya bahari.

(22-43: Mat. 9:18-26; Luk. 8:41-56.)

22Akaja mmoja wao majumbe wa nyumba ya kuombea, jina lake Yairo; alipomwona akamwangukia miguuni pake,

23akambembeleza sana akisema: Kibinti changu yumo kufani; nakuomba, uje, umbandikie mikono, apate kupona na kuwa mzima tena.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help