1Mfalme Dawidi akauambia ule mkutano wote: Mwanangu Salomo, huyu mmoja, Mungu aliyemchagua, ujana wake ungali mchanga bado, nayo kazi hii ni kubwa, kwani si mtu anayejengewa jumba hili tukufu, ila ni Bwana Mungu.
6Ndipo, wakuu wa milango wa wakuu wa mashina ya Waisiraeli na wakuu wa maelfu na wa mamia nao wakuu wa kazi za mfalme walipochanga kwa kupendezwa,
7wakatoa vya kutumiwa nyumbani mwa Mungu vipande vya dhahabu 5000, ndio frasila 15000, na robo za dhahabu 10000, ndio shilingi kama 400000, na vipande vya fedha 10000 kumi, ndio frasila 30000, na vipande vya shaba 18000, ndio frasila 54000, na vipande vya chuma 100000 ndio frasila 300000.
8Nao walioonekana kuwa wenye vito wakavitia katika vilimbiko vya nyumba ya Bwana mkononi mwa Mgersoni Yehieli.Kufa kwake Dawidi.
26Dawidi, mwana wa Isai, alikuwa mfalme wa Waisiraeli wote.
27Nazo siku, alizokuwa mfalme wao Waisiraeli, zilikuwa miaka 40; Heburoni alikaa mwenye ufalme miaka 7, namo Yerusalemu alikaa mwenye ufalme miaka 33.1 Fal. 2:11.
28Akafa mwenye miaka mingi alipokuwa ameshiba siku na mali na macheo, naye mwanawe Salomo akawa mfalme mahali pake.
29Nayo mambo ya mfalme Dawidi, ya kwanza na ya mwisho tunayaona, yameandikwa penye mambo ya mtazamaji Samweli na penye mambo ya mfumbuaji Natani na penye mambo ya mchunguzaji Gadi;1 Mambo 21:9.
30ndimo, yalimo mambo yote ya ufalme wake na ya uwezo wake nazo siku zilizompata yeye na Waisiraeli na nchi zote za kifalme.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.