5 Mose 24 - Swahili Roehl Bible 1937

Cheti cha kuachana.

1Mtu akichukua mwanamke na kumwoa, naye halafu asipompendeza machoni pake, kwa kuwa ameona kwake neno lisilofaa, na amwandikie cheti cha kuachana na kumpa mkononi mwake, kisha na amtume kwenda zake na kutoka nyumbani mwake.

8Jiangalie, utakapopatwa na pigo la ukoma! Yaangalie sana na kuyafanya yote sawasawa, kama watambikaji Walawi watakavyowafunza ninyi! Kama nilivyowaagiza wao, yaangalieni, myafanye vivyo hivyo!

10Utakapomkopesha mwenzako cho chote, alichokukopa, usiingie nyumbani mwake kumtoza roho yake,

11ila usimame nje, yule mtu uliyemkopesha wewe akutolee rehani yake huko nje.

12Naye kama ni mtu mnyonge, usilale na rehani yake,

13ila umrudishie rehani yake, jua litakapokuchwa, apate kulala na nguo yake ya kujifunika, akubariki. Hii itakupatia wongofu machoni pake Bwana Mungu wako.

14Usimkorofishe mtu wa kazi aliye mkiwa na mkosefu wa mali, kama ni wa ndugu zako au mmojawapo wa wageni watakaokaa katika nchi yako malangoni pako,

17Usipotoe shauri la mgeni wala la mwana aliyefiwa na wazazi, wala mjane usimtoze nguo yake kuwa rehani!

19Utakapoyavuna mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda mmoja shambani, usirudi kuuchukua, ila uache, uwe wa mgeni au wa mwana aliyefiwa na wazazi au wa mjane, Bwana Mungu wako akubarikie kazi zote za mikono yako.

20Utakapoupukutisha mchekele wako usiurudie tena kuyapukutisha nayo matawi yake, matunda yao na yawe ya mgeni au ya mwana aliyefiwa na wazazi au ya mjane.

21Utakapochuma mizabibuni kwako, usiirudie mizabibu kuiokoteza. Na iwe ya mgeni au ya mwana aliyefiwa na wazazi au ya mjane.

22Nawe kumbuka, ya kama ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri! Kwa sababu hii mimi ninakuagiza kuyafanya haya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help