2 Timoteo 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Anwani.

1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, nikitangaze kiagio cha uzima uliomo mwake Kristo Yesu, nakuandikia barua, wewe Timoteo, mwanangu mpendwa.

2Upole ukukalie na wema na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu, Bwana wetu!

Roho ya nguvu na ya upendo.

3Namshukuru Mungu, ninayemtambikia tangu siku za baba zangu kwa moyo utakatao kwa kujua mema tu. Nakukumbuka pasipo kukoma nikiomba usiku na mchana.Timoteo sharti afulize kumtegemea Mungu.

12Kwa sababu yake nateseka hivyo, lakini sivionei soni, kwani namjua, nimtegemeaye. Tena ninalo shikizo hili la kwamba: Yuko na nguvu ya kulilinda limbiko langu, mpaka siku ile itakapotimia.

15Neno lile nalijua, ya kuwa wote walioko Asia wameniacha; miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.2 Tim. 4:16.

16Bwana awahurumie wao wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa kuwa amenipoza moyo mara nyingi; hakuwa na soni ya mafungo yangu,

17ila alipofika Roma akajipingia kunitafuta, mpaka akiniona.

18Bwana ampe kuona huruma kwake Bwana siku ile! Nayo yote, aliyonitimikia huko Efeso, wewe umeyatambua kuliko mimi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help