1Ikawa siku nyingine, wana wa Mungu walipokuja kumtokea Bwana, Satani naye akaja katikati yao kumtokea Bwana.
11Rafiki zake Iyobu watatu walipoyasikia hayo mabaya yote yaliyompata, ndipo, walipoondoka kila mtu mahali pake, Elifazi wa Temani na Bildadi wa Sua na Sofari wa Nama, wakapatana kwenda pamoja kumpongeza na kumtuliza moyo.1 Mose 25:2; 36:15; Yos. 15:41; Yer. 49:7.
12Wakayainua macho yao walipokuwa wako mbali bado, lakini hawakumtambua, wakapaza sauti zao, wakalia, wakazirarua nguo zao, kila mtu zake, wakajimwagia mavumbi kichwani na kujielekeza mbinguni.
13Wakakaa pamoja naye chini siku saba mchana kutwa na usiku kucha, hakuna aliyeweza kumwambia neno, kwani waliyaona maumivu yake kuwa makubwa mno.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.