Yohana 14 - Swahili Roehl Bible 1937

Kwenda kwa Baba.

1Mioyo yenu isizizimke! Mtegemeeni Mungu, nami mnitegemee!

2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama visingekuwa hivyo, ningewaambia: Nakwenda kuwatengenezea mahali.

3Nami ijapokuwa ninakwenda kuwatengenezea mahali, nitakuja tena, niwachukue kuwapeleka mwangu, kwamba nanyi mwepo hapo, nilipo mimi.Kiagio cha Roho Mtakatifu.

15*Mkinipenda yashikeni maagizo yangu!

16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa mtuliza mioyo mwingine, akae pamoja nanyi kale na kale.

23*Yesu akajibu, akamwambia: Mtu akinipenda atalishika Neno langu, naye Baba yangu atampenda, nasi tutamfikia, tufanye makao kwake.

25Haya nimewaambia nikingali kwenu.

26Lakini yule mtuliza mioyo, yule Roho Mtakatifu, Baba atakayemtuma katika Jina langu, ndiye atakayewafundisha yote na kuwakumbusha yote, mimi niliyowaambia ninyi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help