Yosua 13 - Swahili Roehl Bible 1937

Mungu anamwagiza Yosua kuwagawia Waisiraeli nchi nzima ya Kanaani.

1Yosua alipokuwa mzee mwenye siku nyingi, Bwana akamwambia: Wewe umekwisha kuwa mzee mwenye siku nyingi, nazo nchi zilizosalia uchukuliwa ni nyingi bado.

2Nazo nchi zilizosalia ni hizi: majimbo yote ya Wafilisti na Gesuri nzima

3toka mto wa Sihori ulioko upande wa Misri mpaka kwenye mipaka ya Ekroni kaskazini; kwani nchi hizo huhesabiwa kuwa za Wakanaani. Nao wakuu wa Wafilisti ni hawa watano: Wa Gaza na Wa Asdodi na wa Askaloni na wa Gati na wa Ekroni.

4Tena Waawi walioko kusini, tena nchi nzima ya Wakanaani na Meara iliyo ya Wasidoni mpaka Afeki hata kwenye mipaka ya Waamori.

5Tena nchi ya Wagebali na ya Libanoni yote upande wa maawioni kwa jua toka Baali-Gadi chini ya milima ya Hermoni, mpaka ufike Hamati.

6Wote wakaao milimani toka Libanoni mpaka Misirefoti-Maimu, wale Wasidoni wote nitawafukuza wote mbele ya wana wa Isiraeli; wewe nchi hizi zigawie tu Waisiraeli na kuzipigia kura, ziwe fungu lao, kama nilivyokuagiza.Nchi za Rubeni na za Gadi na za nusu ya Manase.

15Mose aliwapa wao wa shina la Rubeni nchi ya kuzigawanyia koo zao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help