Ezekieli 16 - Swahili Roehl Bible 1937

Wayerusalemu wanafanana na mwanamke mgoni.(Taz. Ez. 23.)

1Neno la Bwana likanijia la kwamba:

2Mwana wa mtu, wajulishe Wayerusalemu machukizo yao

3ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyouambia Yerusalemu: Nchi ya Kanaani ndiko kwenu kwa mwanzo wako na kwa kuzaliwa kwako; baba yako ni Mwamori, mama yako ni Mhiti.

4Nako kuzaliwa kwako kulikuwa hivyo: siku ulipozaliwa hukukatwa kitovu, wala hukuogoshwa maji, utakate, wala hukupakwa chumvi hata kidogo, wala hukuvikwa nguo za kitoto.

5Halikuwako jicho lililokuonea uchungu wa hukufanyizia moja tu la mambo hayo kwa lililokuonea uchungu wa kukufanyizia moja tu la mambo hayo kwa kukuhurumia, ila ulitupwa shambani, kwa kuwa waliichukia roho yako siku, ulipozaliwa.

6Nikapita hapo, ulipokuwa, nikakuona ulivyogaagaa katika damu yako nikakuambia: Hivyo, unavyolala katika damu yako, uwe mzima! Nikakuambia kweli: Hivyo unavyolala katika damu yako, uwe mzima!

7Nitakupa kuwa maelfu na maelfu, kama majani ya shambani yalivyo mengi. Ndipo, ulipokua na kuendelea hivyo, mpaka ukawa mkubwa, ukapata kuwa mzuri zaidi, maziwa yako yakapata nguvu nazo nywele zako zikaota sana, lakini wewe ulikuwa ungaliko uchi bado pasipo kufunikwa na nguo.

8Nikapita hapo, ulipokuwa, nikakuona, ya kuwa siku zako za kuvunja ungo zimetimia, nikakutandia guo langu la kujifunika, nikaufunika uchi wako, nikakuapia na kukufanya agano na wewe, nawe ukawa wangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help