5 Mose 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Waisiraeli hawakuyashukuru matendo mema ya Mungu.

1Haya ndiyo maneno, Mose aliyowaambia Waisiraeli wote ng'ambo ya huku ya Yordani nyikani kwenye mbuga zinazoielekea Bahari Nyekundu katikati ya Parani na Tofeli na Labani na Haseroti na Di-Dhahabu.

2Kutoka Horebu ulikuwa mwendo wa siku kumi na moja kwa kushika njia ya kwenda mlimani kwa Seiri mpaka Kadesi-Barnea.

3Ikawa siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja katika mwaka wa arobaini, ndipo, Mose alipowaambia wana wa Isiraeli hayo yote, kama Bwana alivyomwagiza kuwaambia.

4Ilikuwa hapo, alipokwisha kumpiga Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni, na Ogi, mfalme wa Basani, aliyekaa Astaroti karibu ya Edirei.

29Ndipo, nilipowaambia ninyi: Msitetemeke, wala msiwaogope!

30Bwana Mungu wenu anayewatangulia, yeye atawapigia vita, matendo yake yawe kama yale yote, aliyowafanyizia kule Misri, mliyoyaona kwa macho yenu.2 Mose 14:14,25; Yos. 10:14.

31Nako nyikani mmeona, Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama mtu anavyomchukua mwanawe, katika hizo safari zote, mlizokwenda, mpaka mkifika mahali hapa.2 Mose 19:4; 5 Mose 8:5.

32Lakini ijapo ameyafanya hayo yote, ninyi hamkuwa mkimtegemea Bwana Mungu wenu.

33Naye alikuwa amewatangulia njiani, awatafutie mahali pa kupigia makambi yenu; aliwatangulia usiku kwa moto, awaangazie hizo njia, mlizokwenda, tena mchana kwa wingu.2 Mose 13:21.

34Hapo, Bwana alipoyasikia yale maneno, mliyoyasema, akachafuka, akaapa kwamba:

35Watu hawa wote wa hiki kizazi kibaya hawataiona kabisa hiyo nchi njema, niliyowaapia baba zao kuwapa,

36Kalebu, mwana wa Yefune, yeye tu ataiingia, nami nitampa nchi hiyo, aliyoikanyaga, iwe yake yeye na ya wanawe, kwa kuwa alimfuata Bwana kwa moyo wote.

37Mimi nami Bwana akanikasirikia kwa ajili yenu, akaniambia: Wewe nawe hutaiingia hiyo nchi.4 Mose 20:12.

38Lakini Yosua, mwana wa Nuni, anayekutumikia, yeye ataingia huko; mshikize moyo, kwani ndiye atakayewagawia Waisiraeli mafungu ya nchi yatakayokuwa yao.4 Mose 34:17.

39Nao watoto wenu, mliowasema, ya kama watakuwa mateka, nao wana wenu wasiojua leo bado kupambanua mema na mabaya, wao ndio watakaoingia huko, nao nitawapa hiyo nchi, waichukue, iwe yao.

40Lakini ninyi geukeni na kuondoka hapa, mrudi nyikani na kushika njia ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu.

41Ndipo, mlipojibu na kuniambia: Tumemkosea Bwana. Sisi na tupande, tupige vita na kuyafanya yote, Bwana Mungu wetu aliyotuagiza. Lakini hapo mlipojifunga mata yenu ya kupigia vita kwa kuwaza, ya kama ni kazi nyepesi kupanda huko milimani,

42Bwana akaniambia: Waambie: Msipande, wala msipige vita! Kwani mimi simo katikati yenu, msije kupigwa mbele ya adui zenu.

43Nilipowaambia hayo, hamkusikia, mkalikataa neno, kinywa cha Bwana kililolisema; mkapanda milimani kwa kujivuna.

44Kwa hiyo Waamori waliokaa kule milimani walipotoka kupigana nanyi, wakawafukuza, kama nyuki wanavyofanya, wakawapiga ninyi huko Seiri, mfike mpaka Horma.

45Mkarudi na kumlilia Bwana, lakini Bwana hakuzisikia sauti zenu, wala hakuwategea ninyi sikio.

46Kwa hiyo mkakaa Kadesi hizo siku nyingi, mlizozikaa huko.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help