1Haya ni maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia aliyekuwa miongoni mwa watambikaji wa Anatoti katika nchi ya Benyamini.
2Neno la Bwana likamjia siku za Yosia, mfalme wa Yuda, mwana wa Amoni, katika mwaka wa kumi na tatu wa ufalme wake.
4Neno la Bwana likanijia kwamba:
11Neno la Bwana likanijia kwamba: Wewe Yeremia, unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona tawi lenye kufunua maua.
12Bwana akaniambia: Umeona vema, kwani mimi nitayafumbua macho, yalilinde Neno langu, nilitimize.
13Neno la Bwana likanijia mara ya pili kwamba: Wewe unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona chungu chenye maji yanayochemka, nao upande wake wa mbele ulioelekea kaskazini umegeuka.
14Bwana akaniambia: Upande wa kaskazini ndiko, mabaya yatakakofunuliwa, yawafikie wote wakaao nchini.
15Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Nitazameni! Ninaiita milango yote ya kifalme wakaao upande wa kaskazini. Nao watakuja, waweke kila mmoja wao kiti chake cha kifalme malangoni mwa Yerusalemu na ng'ambo za kuta zote za boma lake liuzungukalo, hata kwenye miji yote ya Yuda.
16Ndipo, nitakapowatokezea mapatilizo yangu kwa ajili ya ubaya wao wote, kwa kuwa wameniacha wakavukizia miungu mingine, wakatambikia yaliyofanywa na mikono yao.
17Nawe vifunge viuno vyako! Kisha inuka, kawaambie yote, nitakayokuagiza! Usizistuke nyuso zao, nisije kukustusha nyusoni pao!
18Tazama! Mimi nimekuweka leo kuwa ngome ya mji na nguzo ya chuma na boma la shaba, nchi zote zishindwe nao wafalme wa Yuda, nao wakuu wao, nao watambikaji wao, nao watu waliomo katika nchi hii.Yer. 15:20; Ez. 3:8-9.
19Watapigana na wewe, lakini hawatakuweza, kwani mimi niko pamoja na wewe. Ndivyo, asemavyo Bwana, akuponye.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.