Yeremia 28 - Swahili Roehl Bible 1937

Yeremia na mfumbuaji wa uwongo Hanania.

1Ikawa mwaka uleule, ufalme wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ulipoanzia, katika mwezi wa tano wa mwaka wa nne, ndipo, mfumbuaji Hanania, mwana wa Azuri wa Gibeoni, aliponiambia Nyumbani mwa Bwana machoni pao watambikaji napo pao wote wa ukoo huu kwamba:

2Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwamba: Nimeyavunja makongwa ya mfalme wa Babeli.

3Bado miaka miwili ndipo, mimi nitakapovirudisha mahali hapa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alivyovichukua mahali hapa na kuvipeleka Babeli.

12Neno la Bwana likamjia Yeremia, mfumbuaji Hanania alipokwisha kuivunja miti ya kongwa shingoni pake mfumbuaji Yeremia, likamwambia:

13Nenda kumwambia Hanania haya: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Miti ya kongwa, uliyoivunja, ni ya miti tu; lakini mahali pao umeweka miti ya kongwa iliyo ya chuma.

14Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Makongwa ya chuma nimetia shingoni pao haya mataifa yote, wamtumikie Nebukadinesari, mfalme wa Babeli; watamtumikia kweli, nao nyama wa porini nimempa.Yer. 27:6.

15Basi, mfumbuaji Yeremia akamwambia mfumbuaji Hanania: Sikia, Hanania! Bwana hakukutuma, nawe umewaegemeza watu wa ukoo huu mambo ya uwongo.

16Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kweli: Utaniona, nikikutuma kuondoka huku nchini, mwaka huu wewe utakufa, kwani umewakataza watu kumtii Bwana.Yer. 23:14; 29:32.

17Mfumbuaji Hanania akafa mwaka uleule katika mwezi wa saba.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help