Yeremia 32 - Swahili Roehl Bible 1937

Yeremia ananunua shamba Anatoti.

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwake Bwana katika mwaka wa 10 wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ndio mwaka wa 18 wa Nebukadinesari.

2Ilikuwa hapo, vikosi vya mfalme wa Babeli vilipousonga Yerusalemu; naye mfumbuaji Yeremia alikuwa amefungwa uani penye kifungo kilichokuwa kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda.

36Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema sasa kwa ajili ya mji huu, ambao mnasema, ya kuwa umetiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli kwa nguvu za panga na za njaa na za magonjwa mabaya:

37Mtaniona, nikiwakusanya na kuwatoa katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza kwa makali yangu yaliyowaka moto na kwa machafuko makuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwapa kukaa salama.

38Nao watakuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help