Zakaria 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Mwangamizo wa nchi ya Efuraimu.

1Ifungue milango yako, Libanoni, moto uile miangati yako!

Ombolezeni, ninyi mivinje, kwa kuwa miangati imeanguka!

Miti hiyo iliyokuwa yenye utukufu, imeangamizwa!

2Ombolezeni, ninyi mivule ya Basani!

Kwani msitu uliokuwa hauingiliki umeanguka.

3Sikilizeni, wachungaji wanavyolia,

kwa kuwa hayo malisho yao mazuri mno yameangamizwa!

Sikilizeni, wana wa simba wanavyonguruma,

kwani machaka ya Yordani, waliyojivunia, yameangamizwa!

Kondoo wabaya wanamtoa mchungaji Mwema kwa fedha thelathini.

4Hivi ndivyo, Bwana Mungu wangu anavyosema: Wachunge kondoo walio wa kuuawa tu!

5Waliowanunua huwaua pasipo kukora manza; nao waliowauza husema: Atukuzwe Bwana, kwa kuwa nimepata mali! Nao wachungaji wao hawawahurumii.Mchungaji mbaya.

15Bwana akaniambia: Jichukulie tena vyombo vya mchungaji asiyefaa kitu!

16Kwani utaniona, mimi nikiinua katika nchi hii mchungaji asiyewakagua waliotoweka, asiyewatafuta waliopotea, asiyewaponya waliovunjika, asiyewatunza walio wakiwa, lakini nyama za vinono atazila, nazo kwato zao ataziondoa kwa nguvu.

17Yatampata huyo mchungaji wangu asiyefaa, anayewaacha kondoo! Upanga utaupiga mkono wake na jicho lake la kuume, mkono wake ukauke kabisa, nalo jicho lake la kuume lipofuke kabisa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help