Marko 13 - Swahili Roehl Bible 1937

Mambo yatakayokuja.(1-37: Mat. 24; Luk. 21:5-36.)

1Alipotoka Patakatifu, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Mfunzi, yatazame mawe hayo makubwa na majengo hayo makubwa!

2Yesu akamwambia: Je? Wayatazama majengo haya makubwa? Halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.

3Kisha alipokaa mlimani pa michekele kupaelekea Patakatifu, ndipo, Petero na Yakobo na Yohana na Anderea walipomwuliza walipokuwa peke yao wakisema:

4Tuambie, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yote yatakapotimia?

5Yesu akaanza kuwaambia: Angalieni, mtu asiwapoteze!

6Wengi watakuja kwa jina langu na kusema: Mimi ndiye,

7nao watapoteza wengi. Nanyi mtakaposikia vita na mavumi ya vita msivihangaikie! Hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.

8Kwani watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme. Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko, pengine na njaa. Hayo ni mwanzo tu wa uchungu.(9-13: Mat. 10:17-22; Luk. 21:12-17.)

9Lakini ninyi jiangalieni wenyewe! Watawapeleka barazani kwao wakuu namo nyumbani mwa kuombea, mpigwe, kisha mtasimamishwa kwa ajili yangu mbele ya mabwana wakubwa na mbele ya wafalme, mje mnishuhudie kwao.

10Nao Utume mwema sharti utangazwe kwanza kwa mataifa yote.

14Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali pasipompasa; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana! Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani!

28Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.

29Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo, yakiwapo, tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!

30Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma mpaka hapo, yatakapokuwapo hayo yote.

31Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.

32Lakini ile siku au saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba tu.

33Angalieni! Kesheni! Kwani hamjui, siku zake zitakapokuwapo. Vinafanana na mtu mwenye kufunga safari aliyeiacha nyumba yake, akawapa watumishi wake nguvu akimgawia kila mtu kazi yake, naye mlinda mlango akamwagiza, akeshe.

34Basi, hivyo kesheni! Kwani hamjui, mwenye nyumba atakaporudia, kama atakuja jioni au kati ya usiku au jogoo awikapo au mapema.Mat. 25:14; Luk. 19:12.

35Asije na kuwastusha akiwakuta, mmelala.Luk. 12:38.

36Hilo, ninalowaambia ninyi, nawaambia wote: Kesheni!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help