1Sisi sio, Bwana, sisi sio tupaswao na kutukuzwa, ila Jina lako sharti ulipatie utukufu kwa ajili ya upole wako na kwa ajili ya welekevu wako.
3Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, yote yampendezayo huyafanya.
(4-11: Sh. 135:15-20.)4Vinyago vyao ni fedha na dhahabu, mikono ya watu ndiyo iliyovifanya:
12Bwana hutukumbuka, atubariki. Ataubariki mlango wao wa Waisiraeli, ataubariki nao mlango wake Haroni.
13Atawabariki wao wamwogopao Bwana, walio wadogo pamoja nao walio wakubwa.
14Bwana ataendelea kuwafanyia hivyo ninyi nao wana wenu watakaokuwa.
15Ninyi ndio mliobarikiwa naye Bwana aliyezifanya mbingu hata nchi.
16Mbingu ni mbingu zake yeye Bwana, nchi aliwapa wana wa watu.
17Bwana hawamshangilii walio wafu, wala wote walioshukia huko kuliko kimya.Sh. 6:6; Yes. 38:18.
18Lakini sisi na tumkuze Bwana kuanzia sasa, hata kale na kale! Haleluya!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.