1Siku zile Hizikia akaugua, kufa kukamjia karibu. Ndipo, mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi, alipokuja kwake, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Yaliyo yako yaagizie walio wa mlango wako! Kwani wewe utakufa, hutarudi kuwa mzima tena.
2Hizikia akageuka na kuuelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,
3akasema: E Bwana, na uukumbuke mwenendo, nilioufanya mbele yako kwa welekevu, nikayafanya kwa moyo wote mzima, yaliyo mema machoni pako. Kisha Hizikia akalia kilio kikubwa.
12Kituo changu kimeng'olewa,
kikachukuliwa kwangu kama hema la mchungaji;
nimezizinga siku za maisha yangu kama mfuma nguo
azikate penye nyuzi zinazozishika;
mchana utakapokuwa haujawa usiku bado, utanitowesha.
13Nikalia mpaka asubuhi,
maana aliivunja mifupa yangu sawasawa kama simba;
mchana utakapokuwa haujawa usiku bado, utanitowesha.
14Nikalia kama kinega au mbayuwayu
nikapiga kelele kama hua,
macho yangu yakafifia kwa kutazama juu kwamba:
Bwana ninakorofika! Nikomboe!
15Sasa nisemeje? Aliyoniambia, yeye ameyafanya.
Nami nitaendelea na kutulia miaka yangu yote
kwa ajili ya uchungu, roho yangu iliouona.
16Bwana! Kwa maneno kama hayo watu hupata uzima,
nao uzima wa roho yangu umo humo;
nami umeniponya na kunirudisha uzimani.
17Tazama! Uchungu uliokuwa kweli uchungu kwangu
umenipatia utengemano!
Kwa kunipenda wewe umeitoa roho yangu
mle shimoni mwa kutoweka,
kwani makosa yangu yote uliyatupa nyuma yako.
18Kwani kuzimuni siko, wanakokushukuru,
wala waliokufa sio wanaokushangilia,
wala walioshuka shimoni sio wanaoungojea welekevu wako.
19Aliye hai, kweli aliye hai ndiye
atakayekushukuru kama mimi leo.
Baba huwajulisha watoto mambo ya welekevu wako.
20Bwana ndiye aliyetaka kuniokoa;
kwa hiyo na tumpigie mazeze na kumwimbia
Nyumbani mwa Bwana siku zetu zote za kuwapo!
21Kisha Yesaya akasema, walete andazi la kuyu, waliweke juu ya jipu, apate kupona.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.