Mashangilio 121 - Swahili Roehl Bible 1937

Mchungaji mwelekevu wa Isiraeli.Wimbo wa kupapandia Patakatifu.

1Ninayainua macho yangu na kuyaelekeza milimani, kwani ndiko, utakakotoka msaada wangu.

3Hatautoa mguu wako, uje kujikwaa, maana halali usingizi akulindaye.

4Tazameni! Halali usingizi, wala hasinzii yeye aliye mlinzi wake Isiraeli.

5Bwana ndiye akulindaye, Bwana ni kivuli chako kuumeni kwako,

6mchana jua lisikuumize, wala mwezi usiku.

7Bwana atakukingia mabaya yote, atailinda roho yako.4 Mose 6:24.

8Bwana na akulinde kutoka kwako na kuingia kwako kuanzia sasa hata kale na kale!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help