1 Mose 32 - Swahili Roehl Bible 1937

Yakobo anakutana na malaika.

1Yakobo alipokwenda safari yake akakutana na malaika wa Mungu.Yakobo anatafuta mapatano na Esau.

13Kisha akalala huko usiku huo, akatoa katika yale mapato yaliyokuwa mkononi mwake matunzo ya kumpa kaka yake Esau:

14mbuzi majike 200 na madume 20, kondoo majike 200 na madume 20,

15ngamia wanyonyeshao 30 pamoja na wana wao, ng'ombe majike 40 na madume 10, punda majike 20 na wana wa punda 10;

16akawatia mikononi mwa watumwa wake, kundi kwa kundi peke yake, akawaambia hawa watumwa wake: Nitangulieni, tena katikati ya kila makundi mawili acheni nafasi.

17Naye wa kwanza akamwagiza kwamba: Mkubwa wangu Esau atakapokutana na wewe na kukuuliza kwamba: Wewe mtu wa nani? Unakwenda wapi? Nao hao nyama, wanaowatanguliza, ni wa nani?

18Umwambie: Ni wa mtumishi wako Yakobo, ndio matunzo, anayomtumia bwana wangu Esau, naye mwenyewe anatufuata nyuma.

19Naye wa pili na wa tatu nao wote waliowafuata watumwa hawa akawaagiza kwamba: Mtakapomwona Esau mwambieni maneno yayo hayo!

20Kisha semeni nanyi: Naye mtumishi wako Yakobo anatufuata nyuma. Kwani alisema moyoni mwake: Nitaupoza uso wake kwa hayo matunzo yatakayonitangulia; nitakapoonana naye halafu, labda atanipokea vema.

21Kwa hiyo matunzo yakamtangulia, naye akalala usiku huo humo kambini.

Yakobo anashindana na malaika.

22Usiku huo alipoamka akawachukua wakeze wawili na wale vijakazi wawili na wanawe kumi na mmoja, akaenda kuvuka kivukoni kwa Yakobo;

23akawachukua, akawavusha hapo mtoni, akayavusha nayo yote, aliyokuwaa nayo.

24Naye Yakobo mwenyewe akasalia peke yake ng'ambo ya huko. Mara mtu akakamatana naye, mpaka jua lilipopambazuka.Yakobo anaitwa Isiraeli.

27Naye akamwuliza: Jina lako nani? Akasema: Yakobo.1 Mose 35:10.

28Ndipo, aliposema: Hutaitwa tena jina lako Yakobo, ila Isiraeli (Mshinda Mungu), kwani umeshindana na Mungu, hata na watu, ukawashinda.

29Naye Yakobo akamwuliza kwamba: Niambie jina lako! Akamwambia: Jina langu unaliulizia nini? Kisha akambariki hapo.Amu. 13:17-18.

30Yakobo akapaita mahali pale Penieli (Uso wa Mungu) kwamba: Nimeonana na Mungu uso kwa uso, nayo roho yangu ikapona.2 Mose 33:20.

31Alipovuka hapo Penieli, usiku ukamchea, naye alikuwa akichechemea kwa ajili ya kiuno chake.

32Kwa sababu hii wana wa Isiraeli hawali mshipa ulio juu ya nyonga ya kiuno mpaka siku hii ya leo, kwani yule aliigusa nyonga ya kiuno cha Yakobo penye mshipa wa kiuno.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help