Wafilipi 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Upatanisho.

1Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, ninaowatunukia, m furaha yangu na kilemba changu; wapenzi, simameni vivyo hivyo kwake Bwana!Furaha ya Kikristo.

4*Furahini siku zote kwa kuwa wake Bwana! Nasema tena: Furahini!Shukrani.

10Hivyo, nilivyo mwake Bwana, nalifurahi sana, ya kuwa siku hizi mmekwisha pata tena kunitunza mimi. Tangu kale mlikuwa mkiyawaza, lakini siku za kati hamkuweza.

11Sisemi hivyo kwamba: Nimekosa kitu. Kwani mimi nimejifunza kutoshewa na hayo, niliyo nayo.1 Tim. 6:6.

12Najua kupungukiwa, najua kufurikiwa. Po pote mambo yo yote si mgeni nayo, kama ni kushiba au kuona njaa, kama ni kufurikiwa au kukosa.2 Kor. 6:10.

13Nayaweza yote kwa nguvu yake yeye anayenitia nguvu.2 Kor. 12:10.

14Lakini mmefanya vizuri mlipojitoa, mwe wenzangu wa maumivu.

15Nanyi Wafilipi mwajua: tangu hapo, nilipoanza kuutangaza Utume mwema, nilipotoka Makedonia, hakuna wateule wengine walionigawia wakiyatoa yaleyale, waliyopewa, msipokuwa ninyi peke yenu.2 Kor. 11:9.

16Hata nilipokuwa Tesalonike, mmetuma mara ya kwanza na mara ya pili, mkanipa vya kunitunza.

17Sivisemi hivyo kwa maana, nayatafuta matunzo, ila nayatafuta matunda kwamba: Mapato yenu yaongezeke.1 Kor. 9:11.

18Kwani nilikuwa nayo yote yanipasayo, nayo yalikuwa mengi. Kisha nikafurikiwa nilipopewa na Epafurodito vitu vile vilivyotoka kwenu; ni manukato yanukayo vizuri kama ng'ombe ya tambiko ifaayo ya kumpendeza Mungu.Fil. 2:25.

19Mungu wangu awape ninyi, yote mkosayo yawafurikie! Maana yeye ni mwenye mali nyingi zilizomo katika utukufu uliotokea katika Kristo Yesu.

20Yeye Mungu aliye Baba yetu atukuzwe kale na kale pasipo mwisho! Amin.

21Nisalimieni kila mtakatifu aliye wake Kristo Yesu! Ndugu walio pamoja nami wanawasalimu.

22Watakatifu wote wanawasalimu, kupita wengine ni wale waliomo nyumbani mwake Kaisari.

23Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uzikalie roho zenu! Amin.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help