2 Mambo 20 - Swahili Roehl Bible 1937

Yosafati anawashinda Waamoni na Wamoabu.

1Ikawa baada ya hayo, wakaja wana wa Moabu na wana wa Amoni pamoja na Waamoni wengine kumpelekea Yosafati vita.

2Watu wakaja kumpasha Yosafati habari kwamba: Uvumi wa watu wengi unakujia, unatoka ng'ambo ya huko ya bahari upande wa Ushami, nao wamekwisha kufika Hasesoni-Tamari, ndio Engedi.

3Yosafati akaogopa, akamwelekezea Bwana uso wake na kulitafuta shauri lake, akatangaza katika nchi yote ya Yuda, watu wafunge.

4Wayuda wakakusanyika kutafuta msaada kwa Bwana; walipokwisha kufika na kutoka katika miji yote ya Yuda, wamtafute Bwana,Kutawala kwake Yosafati.(20:31—21:1: 1 Fal. 22:41-51.)

31Yosafati akawa mfalme wa Wayuda, naye alikuwa mwenye miaka 35 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 25. Jina la mama yake ni Azuba, binti Silihi.

32Akaendelea kuishika njia ya baba yake Asa, hakuiacha kabisa, akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana.

33Matambiko ya vilimani tu hayakukoma, kwani watu hawajamwelekezea Mungu wa baba zao mioyo yao.

34Mambo mengine ya Yosafati, ya kwanza na ya mwisho, tunayaona, yameandikwa katika mambo ya Yehu, mwana wa Hanani, yaliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli.

Yosafati anafanya maagano na Ahazia.

35Baada ya hayo Yosafati, mfalme wa Wayuda, akajiunga na Ahazia, mfalme wa Waisiraeli; lakini huyu matendo yake, aliyoyafanya, yalikuwa maovu.1 Fal. 22:52-54.

36Akajiunga naye kwa kutengeneza merikebu za kwenda Tarsisi; wakatengeneza merikebu hata huko Esioni-Geberi.

37Eliezeri, mwana wa Dodawa wa Maresa, akamfumbulia Yosafati kwamba: Kwa kuwa umejiunga na Ahazia, Bwana atazivunja hizi kazi zako. Kwa hiyo vyombo vikavunjika, havikuweza kwenda Tarsisi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help