2 Mose 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Kondoo ya Pasaka.(1-28: 2 Mose 23:15; 34:18; 3 Mose 23:5-14; 4 Mose 9:1-14; 28:16-25; 5 Mose 16:1-8; 1 Kor. 5:7)

1Bwana akamwambia Mose na Haroni katika nchi ya Misri kwamba:

2Mezi huu sharti uwawie wa kwanza a miezi, uwe wenu wa kwanza wa kuihesabu miezi ya mwaka.

14Siku hiyo sharti iwe kwenu ya kuikumbuka, mwilie sikukuu ya Bwana. Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijvyo, mwilie sikukuu.

15Siku saba na mle mikate isiyochachwa. Siku ya kwanza sharti mkomeshe chachu na kuziondoa nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula siku ya kwanza mpaka siku ya saba yaliyo yenye chachu sharti huyo ang'olewe kwao Waisiraeli.Waisiraeli wanaanza kutoka Misri.

34Watu wakauchukua unga wao uliokandwa, ukiwa haujachachuka bado, nayo mabakuli yao ya kukandia wakayafunga katika nguo zao, wakayachukua mabegani.

35Nao wana wa Isiraeli walikuwa wameyafanya, Mose aliyowaambia, wakiwatakia Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na nguo.

37Hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyoondoka Ramusesi kwenda Sukoti, nao walikuwa wanawaume tu waliokwenda kwa miguu 600000 pasipo watoto.

38Nao wengine wengi waliochanganyika nao wakapanda nao, tena mbuzi na kondoo na ng'ombe, kundi kubwa sana.

39Nao ule unga uliokandwa, waliouchukua walipotoka Misri, wakauoka kuwa maandazi na mikate isiyochachwa, kwani ulikuwa haukuchachuka, kwani walikimbizwa kutoka Misri, hawakuweza kukawilia wala kutengeneza pamba za njiani.

40Miaka ya kukaa, wana wa Isiraeli waliyokaa Misri, ilikuwa miaka 430.1 Mose 15:13.

41Hii miaka 430 ilipokwisha pita, siku iyo hiyo vikosi vyote vya Bwana vilitoka katika nchi ya Misri.

42Usiku huo wa kuwatoa katika nchi ya Misri ulikuwa usiku wa Bwana wa kuangaliwa; kwa hiyo usiku huo wa Bwana na uwe wa kuangaliwa kwa wana wote wa Isiraeli na kwa vizazi vyao vijavyo.

Maongozi ya sikukuu ya Pasaka.

43Bwana akamwambia Mose na Haroni: Haya ndiyo maongozi ya Pasaka: mtu asiye wa kwenu asiile!

44Lakini kila mtumwa aliyenunuliwa kwa fedha ataila, ukiisha kumtahiri.

45Atakayekaa tu kwako na mtu wa mshahara asiile!

46Sharti iliwe katika kila nyumba, lakini usitoe nyama yake yo yote mle nyumbani na kuipeleka nje, wala msimvunje mfupa wo wote!Yoh. 19:36.

47Wao wote wa mkutano wa Waisiraeli sharti wafanye hivyo.

48kama mgeni anakaa ugenini kwako, naye akitaka kuila Pasaka ya Bwana, uwatahiri wote walio wa kiume kwake, kisha ataweza kuikaribia kuila, maana atakua kama mzalia wa hiyo nchi, lakini kila asiyetahiriwa asiile!

49Maonyo yawe yayo hayo ya mzalia wa kwenu nayo ya mgeni atakayekaa ugenini kwako!3 Mose 24:22.

50Nao wana wa Isiraeli wote wakayafanya; kama Bwana alivyomwagiza Mose na Haroni, ndivyo, walivyofanya.

51Ilikuwa siku ileile moja tu, Bwana akiwatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri vikosi kwa vikosi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help