Ezekieli 21 - Swahili Roehl Bible 1937

Panga za Wakasidi zitawajia Wayudana Waamoni.

1Neno la Bwana likanijia la kwamba:

2Mwana wa mtu, uelekeze uso wako kuutazama Yerusalemu, upatangazie Patakatifu na kuifumbulia nchi ya Isiraeli yatakayokuwa!

3Iambie nchi ya Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaona, nikikujia na kuuchomoa upanga wangu alani mwake, niangamize waongofu na wapotovu, watoweke kwako.

4Kwa kuwa nitaangamiza waongofu na wapotovu, watoweke kwako, kwa hiyo upanga wangu utachomolewa alani mwake, uwapige wote wenye miili toka kusini hata kasikazini.

5Ndipo, wote wenye miili watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, ya kuwa nimeuchomoa upanga wangu alani mwake, usirudi humo tena.

6Lakini wewe mwana wa mtu, piga kite! Kwa viuno vilivyovunjika na kwa uchungu ulio mkali piga kite, wakuone!

7Tena wakikuuliza: Unapiga kite? uwaambie: Kwa hayo, niliyoyasikia, ya kuwa yatakuja, moyo wote umeyeyuka, nayo mikono ikalegea, nayo roho yote ikazimia, nayo magoti yakaja kugeuka kuwa kama maji. Mtaona, yakija kutimia; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.

8Neno la Bwana likanijia la kwamba:

9Mwana wa mtu, yafumbue yatakayokuwa ukisema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Sema: Uko upanga, ni upanga mwenyewe, umenolewa na kusuguliwa vema.

28Nawe mwana wa mtu, yafumbue yatakayokuwa ukisema: Haya ndiyo Bwana Mungu anayowaambia wana wa Amoni kwa ajili ya matusi yao, sema: Upanga ulio upanga kweli umechomolewa, nao umesuguliwa, upate kuchinja na kuua kabisa, kusudi uwe kama umeme.Ez. 25:2-7.

29Lakini wamekutazamia maono yasiyokuwa, wakakuagulia uwongo, wakuvute, uje kuwapiga shingo zao waliojipatia uchafu na kuacha kunicha, kwamba siku yao imetimia, kwa kuwa ni wakati wa mwisho wa kukora manza.

30Lakini urudishe huo upanga alani mwake! Mahali, ulipoumbwa katika nchi, ulikozaliwa, nitakukatia shauri.

31Nitakumwagia makali yangu, kwa moto wa machafuko yangu nitakufokea, kisha nitakutia mikononi mwa watu wasio wa kimtu, walio mafundi wa maangamizo.

32Utakuwa chakula cha moto, damu yako itamwagwa katika nchi yako katikati, hutakumbukwa tena, kwani mimi Bwana nimeyasema.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help