1Hili ni neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beri, Uzia na Yotamu na Ahazi na Hizikia walipokuwa wafalme wa Wayuda, naye Yoroboamu, mwana wa Yoasi, alipokuwa mfalme wa Waisiraeli.
2Hapo, Bwana alipoanza kusema na Hosea, Bwana akamwambia Hosea: Nenda, ujichukulie mwamamke mgoni, ujipatie nao watoto wa ugoni! Kwani nchi hii inafuata ugoni kwa kumwacha Bwana.
3Akaenda, akamchukua Gomeri, binti Dibulemu; naye akapata mimba, akamzalia mwana wa kiume.
4Bwana akamwambia: Mwite jina lake Izireeli! Kwani kiko bado kitambo kidogo, ndipo, nitakapoulipisha mlango wa Yehu damu za Izireeli na kuukomesha ufalme wa Isiraeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.